Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea udiwani aahidi gereza la ghorofa, barabara za juu

9467 Diwani+pic TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Kati ya wagombea udiwani katika kata ya Mawenzi Moshi mjini ambao huwezi kuchoka kuwasikiliza kutokana na ahadi zao, ni mgombea wa chama cha Sauti ya Umma (Sau), Issack Kireti.

Akihutubia jana jioni Julai 31, 2018 katika mkutano wa hadhara ofisi ya zamani ya Kata ya Mawenzi, Kireti ameahidi kujenga magereza yenye jengo la ghorofa maalum kwa ajili ya wafungwa wa makosa ya rushwa na ufisadi.

Kireti ambaye alionekana kama anahutubia wapita njia zaidi, amesema jengo hilo la magereza litakuwa ni la ghorofa na litakuwa na bwawa la kuogelea na wafungwa wataruhusiwa kukutana na wake zao.

“Nilipokuwa nagombea ubunge 2015 nililiahidi hili na leo nataka niwaahidi tena mkinichagua kuwa diwani nitapigania kujengwa kwa gereza la ghorofa kwa ajili ya mafisadi na wala rushwa,”amesema.

Lakini hakuishia hapo, kwani alikuja na ahadi nyingine kubwa zaidi ambapo aliahidi kujenga barabara za juu (flyovers) kwa ajili ya kuwaepusha watembea kwa miguu na ajali za bodaboda.

“Kumekuwa na ajali nyingi za bodaboda wakati watembea kwa miguu wakivuka barabara. Nitakomesha hili kwa kujenga flyovers barabara muhimu ili tuondoe alama za pundamilia,”alidai.

Katika mkutano huo ambao hapakuwepo msemaji mwingine yeyote zaidi yake, mgombea huyo aliahidi kupanda miti katika hospitali ya mawenzi ili wagonjwa wawe wanakula matunda bila kununua.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz