Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea ubunge NRA Monduli, aahidi malambo kila kata

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Mgombea ubunge katika jimbo la Monduli, kwa tiketi ya Chama cha NRA, Feruz Juma Feruz, amewataka wakazi wa jimbo hilo, kumchagua kuwa mbunge kwani anahakikisha, kila kata inachimbiwa bwawa la maji ya mifugo.

Akizungumza na mwananchi, Feruz alisema, tayari amepata wafadhili watakaomsaidia kuchimba mabwawa ya mifugo, katika kata zote ili kutatua kero za wafugaji wilayani Monduli.

"Nawaomba wanichague kuwa mbunge najua kero kubwa ya wananchi ni maji ya kunywa na mifugo na tayari nimepata wafadhili wa kunisaidia," alisema.

Feruz alisema, pia atahakikisha kila kata inapata huduma za maji ili kuondoa kero kwa wananchi.

Akizungumzia mfumo wa kampeni zake, alisema anafanya kampeni za kisasa za nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na mikutano na ana imani atachaguliwa.

"Mimi ndiye mtu sahihi wa kuwa mbunge wa Monduli, naomba wananchi wanipe ridhaa yao," alisema.

Katika uchaguzi wa Monduli vyama vinane vinashiriki na uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Chadema, Julius Kalanga kujiuzulu na kujiunga na CCM.

Chanzo: mwananchi.co.tz