Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea pekee CCM aendelea na kampeni bila kuwa na mshindani

10520 Pic+mgombea TanzaniaWeb

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Muleba. Wafuasi wa CCM katika Kata ya Nyakabango Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wameendelea kupita nyumba kwa nyumba kumnadi mgombea udiwani, Pastory Makunza licha ya mpinzani wake pekee kutoka Chadema kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi utakaofanyika Jumapili Agosti 12.

Diwani wa Kata ya Kimwani, Daudi Kiluma alilazimika jana kutembelea vijiji vya Katembe, Nyakabango na katika soko la Magarini kumnadi Makunza ili wananchi wamuunge mkono katika kuhamasisha wananchi kuleta maendeleo.

Kiluma alisema kata ya Nyakabango itakuwa imepata kiongozi shupavu na mahiri wa kujali na kutetea haki za wananchi.

“Nikiwa na Makunza katika vikao vya baraza, tutashirikiana kuishauri serikali kuweka mazingira mazuri ya wananchi kupata soko la samaki ambao tumeanza kufuata sheria kwa kuacha uvuvi haramu na kutengenezewa barabara za kufika katika vituo vya huduma mbalimbali,” alisema Kiluma.

Mgombea huyo alisema kujitoa kwa mgombea wa Chadema hakuwezi kumfanya aridhike na kuacha kuwatembelea wakazi wa vijiji vitano vinavyounda kata hiyo kubaini matatizo yao na kuweka mikakati ya kuyatatua. Uongozi wa CCM wilayani Muleba ulithibitisha kupokea barua ya kumtangaza Makunza kuwa diwani baada ya kupita bila kupingwa.

Alisema wanawake, wazee, watu wenye mahitaji maalum na watoto chini ya miaka mitano wanahitaji huduma za afya hivyo atahamasisha ujenzi wa kituo cha afya katani humo badala ya kutegemea kituo cha afya Kimeya na kutumia kati ya Sh50,000 na Sh100,000 kukodi gari la mgonjwa.

Hata hivyo, wafuasi wa Chadema walionekana kupeperusha bendera za chama chao wakitoa sauti za kudai imefanyika hujuma mpaka mgombea wao kujitoa na kwamba hawatakata tamaa katika uchaguzi wa mwaka 2020 wanamwandaa mwingine wa kuchuana na CCM.

Chanzo: mwananchi.co.tz