Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea TLP ajipanga kuikomboa Kibamba

B1e585c53ebd375da9c770b9cacb382e.png Mgombea TLP ajipanga kuikomboa Kibamba

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Vijana wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Aivan Maganza amesema anagombea ubunge ili kulikomboa jimbo la Kibamba, Dar es Salaam kwa kuwa lipo nyuma kimaendeleo.

Aliyasema hayo baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na kusisitiza kuwa endapo atashinda atashirikiana na Rais John Magufuli kuwaletea maendeleo wananchi kwa kuwa analifaha mu eneo hilo na changamoto zilizopo.

“Nakishukuru chama changu kwa kunituma kuja kugombea jimbo hili ambalo wananchi wake walikuwa wakiniomba nije kugombea. Hii ni heshima kubwa kwangu na ninajisikia vizuri kuingia katika mchakato huu ambao utaniwezesha kuwa Mbunge hivyo kuwa karibu na Serikali katika masuala ya kimaendeleo” alisema Maganza.

Alisema pamoja na TLP kumuunga mkono Rais Magufuli katika nafasi ya urais, wameokubaliana kugombea ubunge na udiwani katika majimbo yote kwa lengo la kupata nafasi zitakawawezesha kwenda kumsaidia Rais katika kuliletea Taifa maendeleo.

Alisema kupitia uwakilishi wake atashirikiana na TLP kuibadilisha Kibamba kwa kuwa wana dhamira ya dhati kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo. Mbunge aliyemaliza muda wake ni John Mnyika kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Chanzo: habarileo.co.tz