Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea NCCR-Mageuzi amchambua Zitto

E7e29356528fc24e915aada7a90fbb50.png Mgombea NCCR-Mageuzi amchambua Zitto

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimewahadharisha wapiga kura nchini dhidi ya wagombea wanaojali maslahi yao, badala yake wachague wagombea wanaoguswa na matatizo ya wananchi.

Mgombea uraisi wa chama hicho, Yeremia Maganja alitoa hadhari hiyo katika mikutano mbalimbali ya kampeni aliyofanya mkoani Kigoma.

Alisema wagombea wengi wa vyama vya upinzania hawana dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania zaidi ya kuangalia maslahi yao.

Akiwa katika jimbo la Kigoma Mjini, Maganja aliwataka wananchi kutomchagua mgombea ubugne wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto akimtaja kuwa haguswi na matatizo ya wananchi wa jimbo hilokwa kuzingatia miaka mitano aliyokuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema Zitto ameshindwa kutumia ushawishi wake kama Kiongozi Mkuu wa chama, mbunge na chama chenye madiwani wengi katika manispaa ya Kigoma Ujiji.

Alisema badala yake, madiwani wa chama hicho wametumia muda mwingi kugombea madaraka na kutengeneza dili za kupata fedha kupitia miradi inayotekelezwa kwa fedha za serikali.

Maganja alisema kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia kwenye chama hicho wana dhamira ya dhati ya kuwatumikia na kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kushughulikia kero na changamoto zao ambazo zimeshindwa kupata ufumbuzi tangu nchi ipate uhuru.

Mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Wiston Mogha alisema akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atasimamia mkoa wa Kigoma kutumia fursa zilizopo za kibiashara kwenye nchi za ukanda wa maziwa makuu na kuufanya kuwa mkoa wa kimkakati kibiashara.

Mogha alisema kuwa baraza la madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji linaloongozwa na idadi kubwa na madiwani wa chama cha ACT Wazalendo, imeshindwa kushawishi serikali na kubuni miradi ya kiuchumi itakayosaidia kuongeza mzunguko wa fedha na kuinua uchumi wa mkoa.

Alisema wamekuwa wakigombana kwa kutuhumiana kwa ufisadi wa fedha za miradi.

Chanzo: habarileo.co.tz