Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea Chadema atoa neno baada ya kushinda rufaa NEC

11931 Pic+mgombea TanzaniaWeb

Sun, 22 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarime. Mgombea udiwani wa Chadema kata ya Turwa wilayani Tarime, Charles Mnanka ameshinda rufaa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jana Julai 21, 2018 ilisema kati ya rufaa 25 zilizokatwa na wagombea wa udiwani, kumi wameshinda na 15 wameenguliwa kushiriki uchaguzi mdogo wa Agosti 12, 2018.

"Namshukuru Mungu kwa kuona udhalimu niliokuwa ninatendewa na kuutupilia mbali, Ee bwana uhimidiwe," amesema Mnanka alipozungumza na MCL Digital leo Julai 22, 2018.

Mnanka pamoja na wagombea wengine wawili wa NCCR Mageuzi na ACT Wazalendo waliwekewa pingamizi ikidaiwa hawajakidhi vigezo vya kuteuliwa kuwa wagombea.

Mgombea wa CCM, Chacha Kamanda alitangazwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa alipita bila kupingwa.

Waliowekewa pingamizi walidaiwa kuandika majina yao badala ya saini na Mahakama ilipiga muhuri nyuma ya picha zao.

Kutokana na uamuzi wa NEC, Baadaye leo Julai 22, 2018 mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko na Mnanka watapokewa eneo la Mika wakitokea jijini Mwanza.

Uchaguzi katika kata ya Turwa unafanyika baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Zakayo Chacha  (Chadema) kujiuzulu na kujiunga na CCM akieleza ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Rais.

Chanzo: mwananchi.co.tz