Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea Chadema ataka ridhaa kuleta mabadiliko

F142d0bef2b3bc500cccc408fd4e2d4f Mgombea Chadema ataka ridhaa kuleta mabadiliko

Mon, 12 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Aisha Madoga na diwani wa kata ya Uhuru, Salma Mombo, wamewaomba wakazi wa Dodoma kuwapa ridhaa ya kushika nafasi hizo, ili wakaweze kutatua kero ya ardhi ambayo imekuwa sugu kwa miaka mingi.

Wagombea hao kwa pamoja wameomba ridhaa hiyo wakati walipokuwa wakizungumza na wananchi kwenye mkutano wa kampeni wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliofanyika jana viwanja vya Kata ya Uhuru Jijini Dodoma.

Akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni mgombea huyo wa ubunge, alisema akichaguliwa yeye na diwani kushika nafasi hizo atahakikisha anasimamia ardhi ambayo hivi sasa imekuwa kero kutokana na kuwapo kwa kesi nyingi kwenye mabaraza ya kata na mahakama mbalimbali migogoro ya kesi nyingi ambazo zisizotatulika.

Aliwataka wakazi wa Dodoma kutofanya makosa kwa kuchagua viongozi ambao wanafanya kazi zao kwa mazoea bila kujali changamoto zilizopo, bali waende wakafanye chaguo lililo sahihi.

“Mkituchagua mimi na diwani wa kata ya uhuru wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,tutaenda kusimamia kodi ya ardhi ya kila mwana Dodoma ili aweze kupata haki yake ya umiliki kwa uhuru na haki hii na pamoja na urasilimishaji wa ardhi,”alisema.

Naye mgombea udiwani, Salma Mambo aliwaomba wakazi wa mtaa wa Uhuru kumpa ridhaa kwa kumchagua, ili aweze kurudisha eneo la kiwanja cha kuchezea mpira cha shule ya msingi ya Uhuru ambacho jiji limeamua kukifanya kuwa stendi ya malori ya kushusha mizigo.

Alisema kuwa pamoja na kusimamia maendeleo kwenye kata hiyo ya Uhuru atahakikisha anarudisha eneo hilo lililogeuzwa kuwa stendi ya malori ya kushushia mizigo huku wanafunzi wakikosa kiwanja cha kuchezea michezo mbalimbali.

Chanzo: habarileo.co.tz