Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea Chadema asimamishwa kampeni siku 3

Fe6964d1825e0dd5e1978c629968af62 Mgombea Chadema asimamishwa kampeni siku 3

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMATI ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Jimbo la Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa,

imemsimamisha mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Shadrack Malila asifanye kampeni kwa siku tatu kuanzia jana.

Kamati hiyo imesema imechukua hatua hiyo kutokana na mgombea huyo kutoa kauli za uchochezi na maudhi katika moja ya kampeni zake za uchaguzi.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, leo Malila atakabidhiwa barua kumjulisha kuhusu uamuzi huo ili aanze kutumikia adhabu hiyo. Malila pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa.

Mgombea huyo alisema mwakilishi wake aliyehudhuria kikao cha Kamati ya Maadili, amempa taarifa kuhusu adhabu hiyo na kwamba ataipinga kwa madai kuwa ni batili.

"Nikikabidhiwa rasmi barua hiyo na kuisoma ndipo nitatoa uamuzi wa kuendelea na kampeni zangu au nitasitisha,” alisema.

Hiyo ni mara ya pili kwa mgombea huyo kuwania ubunge katika jimbo hilo. Mara ya kwanza ilikuwa 2015 na alishindwa.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu anachuana na mbunge aliyemaliza muda wake, Aeshi Hilaly wa CCM, Doris Kafuku (NCCR-Mageuzi), Julius Mizengo (CUF), Michael Lubava (UDP) na Suleiman Sinani wa ACT-Wazalendo.

Chanzo: habarileo.co.tz