Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea CCM ajinadi ananguvu za kiume

B2276826 293A 48E4 969D CC271385352A.jpeg Mgombea CCM ajinadi ananguvu za kiume

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mgombe huyo, Chris Madaha ametoa kauli hiyo jana Oktoba Mosi, 2022 wakati akiomba kura mbele ya wajumbe 1,344 walioshiriki mkutano huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Madaha ambaye aliomba kura kupitia kundi la vijana, amesema amekamilika kwa sehemu zote na ana nguvu za aina mbili ambazo ni za kimwili na kiume.

“Ndugu wajumbe, mimi nimepewa namba mbili ambayo ni namba ya ushindi, lakini nina nguvu za aina mbili ambazo ni nguvu za kimwili na kiume, nipeni kura zetu,” amesema Madaha.

Kauli hiyo ilisababisha vicheko vya wajumbe na kusababisha zogo lakini waliponyamaza aliyarudia maneno yake mara mbili.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Jabir Shekimweri alimuomba mgombea kipaza sauti na kumtaka akapumzike wakati watu wakiendelea kucheka.

Uchaguzi wa CCM wilaya ulihusisha nafasi ya mwenyekiti, wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa, mkutano wa mkoa na wajumbe wa halmashauri kupitia makundi ya wazazi, vijana na wanawake.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz