Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea CCM aahidi kupeleka mabasi ya mwendo kasi Segerea

48353cdcf9e58f3bcaf5e13f810a1069 Mgombea CCM aahidi kupeleka mabasi ya mwendo kasi Segerea

Sun, 18 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bonah Kamoli amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge ataelekeza maendeleo Kata ya Kimanga kwa kujenga barabara ya mwendo kasi kwa ajili ya mabasi ya haraka na vituo vya afya.

Alisema hayo wakati akifanya kampeni kwenye Kata ya Kimanga alipokuwa akitambulishwa kwa wananchi na katibu wa CCM wilaya ya Ilala, Idd Mkoa.

Aliwaeleza wananchi hayo yote yatatekelezeka endapo watamchagua diwani wa CCM katika kata hiyo, Pastory Kombya ili washirikiane kufanikisha maendeleo hayo ya kata pamoja na jimbo hilo.

“Nitakapochaguliwa mbunge wa Jimbo ili na diwani wangu tutawajengea kituo cha afya, kituo cha daladala cha kisasa, pamoja na barabara ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART),” alisema.

Kombya alisema maendeleo ya kata hiyo yalikuwa yakielekezwa kwenye kata nyingine kwa kuwa diwani aliyemaliza muda wake alikuwa akidaiwa kukwamisha maendeleo, hivyo fedha zilizokuwa zikitolewa na serikali zilielekezwa kwenye kata nyingine ilhali kata ya Kimanga ikirudi nyuma kimaendeleo.

Akizungumzia mikakati yake katika kata ya Kimanga alisema atasimamia yote yaliyopo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2025 ikiwemo kuboresha miundombinu pamoja na sekta ya maji.

Pia atasimamia vikundi vya jimbo la Segerea kuviwezesha mikopo ili viweze kujishughulisha katika uzalishaji kiuchumi. Aliwaomba wananchi hao kumpigia kura mgombea urais wa CCM, John Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo hilo pamoja na diwani.

Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Idd Mkoa aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kuipigia kura CCM kwa ajili ya maendeleo yao.

Alisema CCM imejipanga vizuri katika kushinda majimbo yake yote matatu kwani familia hiyo ni kubwa ina historia nzuri katika utendaji wake wa kazi

Chanzo: habarileo.co.tz