Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea ACTWazalendo na kampeni nyumba kwa nyumba

1403e12edb0483c708d2b2dd307a6320 Mgombea ACTWazalendo na kampeni nyumba kwa nyumba

Thu, 8 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA wa udiwani wa Kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro kupitia Chama cha ACTWazalendo, Vinnie Mtingwa, ameamua kuendesha kampeni ya uchaguzi kwa kupita nyumba kwa nyumba kuomba kura na kuelezea sera za chama chake kabla ya kuanza kampeni za kupanda jukwaani.

Mtingwa alisema hayo wakati akizungumza na HabariLEO jana kuhusu maendeleo ya kampeni za chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

“Mimi nafanya kwanza kampeni za nyumba kwa nyumba na nitamalizia kampeni ya jukwaani,” alisema Vinnie.

Mgombea udiwani wa kata hiyo, alitaja vipaumbele vyake ni pamoja na ushirikishwaji wananchi katika mambo muhimu kama vile kushughulikia kero za malipo ya usombaji wa taka ndani ya kata, uboreshaji wa utoaji wa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Alitaja eneo lingine atakalolishughulikia endapo wananchi wa kata hiyo watamchangua kuwa diwani wao atashughulikia utatuzi wa changamoto za ardhi za wananchi wanaishi eneo la kota ambayo inadaiwa kuuzwa bila wahusika kulezwa lolote.

Chanzo: habarileo.co.tz