Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea ACTWazalendo atoa sababu kuchelewa kampeni

864566c65979e36099f2a83db3ec035e.jpeg Mgombea ACTWazalendo atoa sababu kuchelewa kampeni

Wed, 9 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA udiwani kwa tiketi ya chama cha ACT- Wazalendo katika Kata ya Mbuyuni jimboni Songwe, Daudi Mpakasya ameeleza sababu za kuchelewa kuanza kampeni akisema ni pamoja na kusubiri kujua kama wamewekewa pingamizi.

Katika mazungumzo na HabariLEO juzi mintarafu uzinduzi wa kampeni za wagombea udiwani wa Jimbo la Songwe uliokuwa ufanyike katika Kata ya Mbuyuni mkoani Songwe, Mpakasya alisema, chama wamechelewa kuanza kampeni kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusubiri kujua kama wamewekewa pingamizi, au la.

Hadi tunakwenda mitamboni jana, haikufahamika mara moja kama uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mawasiliano wa ACTWazalendo katika Mkoa wa Songwe, Michael Nyilawila ulifanyika.

Kwa upande wake, Nyilawila alisema chama hicho kimejiandaa kushinda katika kata zote huku akisisitiza usawa kwa wasimamizi wa uchaguzi kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa Mpakasya, hadi juzi wagombea wa vyama vitatu vya CCM, Chadema na ACT-Wazalendo ndio walikuwa wameteuliwa rasmi.

Chanzo: habarileo.co.tz