Dodoma. Mgombea wa nafasi ya uenyekiti mtaa wa Njedengwa kata ya Makulu Jijini Dodoma kwa tiketi ya CCM Daimu Haji amepita bili kupingwa baada ya mgombea wa chama cha AAFP kujitoa dakika za mwisho.
Akizungumzia na Mwananchi leo Novemba 24, 2019, mgombea huyo wa CCM, Daimu, amesema jana alikuwa akiendelea na kampeni na ilipofikia majira ya Saa 12 kasoro jioni akapata taarifa za mgombea huyo kujitoa kwenye uchaguzi.
Haji mesema mgombea huyo alikuwa ni miongoni mwa waliojitokeza kugombea nafasi hiyo kupitia chama cha CCM na baada ya kuenguliwa kwenye kura za maoni akaamua kuhamia chama cha AAFP na kupewa nafasi ya kupeperushi bendera ya chama hicho.
"Nahisi sababu kubwa ya kujitoa ni kutokana na kukosa watu kwenye kampeni, tofauti na ilivyokuwa CCM, " amesema Haji.
Juhudi za kumtafuta mgombea wa AAFP ili azungumzie sababu za kujitoa kwenye uchaguzi huo zinaendelea .