Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meya wa Mikindani Mtwara ajiuzulu

49032 Pic+meya

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tandika na Meya wa Manispaa ya Mikindani Mtwara Mjini, Jofrey Mwanchisye amejiuzulu nyadhifa hizo na kujiunga na CCM.

Mbali na Mwanchisye, diwani mwingine wa Kata ya Chikongola wilayani humo Mussa Namtema naye amejiuzulu wadhifa huo na kujiunga na chama hicho.

Hatua ya Mwanchisye imekuja baada ya kupita siku tano kwa aliyekuwa Meya wa Ilala na Diwani wa Bonyokwa (Chadema), Charles Kuyeko kujiuzulu nyadhifa hizo na kujiunga na CCM akisema ameridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Mwanachisye na Namtema wametangaza uamuzi huo, leo Jumatano Machi 27, 2019 katika ofisi za CCM Mtwara Mjini zilizopo Kata ya Raha leo.

Akizungumza na Mwananchi Mwanchisye amesema “Nilichokifanya sioni dhambi ni jambo la kawaida hasa ukiona huridhishwi na masuala yanayokwenda katika chama ulichokuwa,” amesema na kuongeza kuwa anakwenda CCM kwa sababu ni salama.

Kwa upande wake Namtema amesema naye amejiuzulu ili kujiunga na CCM kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli.

Alipotafutwa Naibu Katibu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya amesema bado hajapata taarifa hizo huku akiahidi kuifuatilia kwa kina ili apate uhakika.

Mbali na Sakaya, mwingine aliyetafutwa ni Makamu Mwenyekiti CUF Bara, Maftaha Nachuma ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Mjini aliyesema hana taarifa, ingawa amezikisikia na kuziona kwenye mitandao ya kijamii.

“Nipo kwenye vikao Dodoma, nimeziona taarifa hizo katika mitandao ya kijamii, ila walikuwa na mwelekeo huo siku nyingi na walikuwa wakiusubiri muda,”amesema Maftaha.



Chanzo: mwananchi.co.tz