Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Membe arejea CCM rasmi, akabidhiwa kadi, ataja sababu za kurejea

Membe Lindi CCM Shaka Bernard Membe

Sun, 29 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ALIYEKUWA mgombea Urais katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe ameeleza sababu zilizomfanya arejee CCM ikiwemo kuondoka kwa sababu ambayo ilimfanya atimkie upinzani.

Membe amekabidhiwa Kadi yake Mpya ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi,Shaka Hamdu Shaka leo Jumapili, Mei 29, 2022, katika Mkutano wa Mbunge jimbo la Mtama, Nape Nnauye katika Kijiji cha Rondo,mkoani Lindi.

"Sababu ambazo zilinifanya niondoke CCM haziko tena. Nimerudi, namshukuru Mwenyekiti wa CCM na wajumbe wa Kamati Kuu kunirudisha. Nimerudi kwenye Chama ambacho nimezaliwa na kukulia, chama ambacho kimenisomesha, nitafia CCM.

“Nilipoondolewa CCM nilisikitika sana, nilisonekana sana, na ninyi wananchi mlisikitika, mlisononekana.

"Nimerejea CCM kwa sababu kuu mbili, sababu ya kwanza nilishauriwa na viongozi wa dini zote, nilishauriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkoa, nilishauriwa na marafiki zangu wote nirejee CCM, nilishauriwa na wana CCM," amesema Bernard Membe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live