Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Membe: Huyu sio Membe yule, subirini muone

Membe Ccm Dodoma Membe: Huyu sio Membe yule, subirini muone

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Benard Membe amesema huu si wakati wa kuzungumza.

Membe ambaye jana Alhamis Machi 31, 2022 CCM ilitangaza kumrudisha kundini, leo Ijumaa Aprili 1, 2022 ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum na alipotoka nje alizongwa na waandishi wa habari wakimtaka aseme neno kuhusu kurejea kwake ndani ya CCM.

Hata hivyo, wakati wote alisema "aaaaa, hapana hapana hapana, Membe huyu siyo yule, subirini mkutano uishe kwanza."

Nje ya mkutano nguli huyo wa siasa alizongwa na kundi kubwa la wajumbe na muda mwingi alikuwa na mbunge wa Iringa mjini Jesca Msambatavangu.

Hata hivyo, baada ya kuzongwa zaidi baadhi ya vijana wa CCM walimfuata na kumshika mkono kisha wakaingia naye ndani huku wakiwafukuza waandishi wa habari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live