Dar es salaam. Wabunge watatu wa Chadema wametoka gereza la Segerea leo Jumatano Machi 12, 2020 baada ya jana kushindikana kutokana na sababu mbalimbali.
Wabunge hao ni Esther Matiko (Tarime Mjini), Ester Bulaya (Bunda) na Halima Mdee (Kawe).
Viongozi wanane wa Chadema pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.
Washtakiwa hao wakiongozwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe walilazimika kwenda jela baada ya kushindwa kukamilisha taratibu za kulipa faini hiyo waliyohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Baada ya hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Chadema walianza kuchangishana fedha kwa ajili ya kuwalipia faini viongozi wake hao.
Hadi jana mchana Chadema walikuwa wamechangisha Sh234 milioni na kutumia Sh110 milioni kuwalipia wabunge hao watatu ambao jana ilishindikana kutoka, sasa wametoka leo. CCM walimlipia Dk Mashinji Sh30 milioni na alitoka jana.
Habari zinazohusiana na hii
- Mdee, Bulaya na Matiko washindwa kutoka jela
- Chadema yakusanya Sh234.6 milioni kuwatoa kina Mbowe
- Chadema waanza mchakato kuwatoa gerezani Halima Mdee, Matiko na Bulaya
- Zitto awachangia Chadema Sh2 milioni