Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Msigwa atoa somo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

64553 Msigwa+pic

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amewataka wakazi wa Iringa kuhakikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa Oktoba 2019 wasiruhusu mtu yeyote kuwachagulia mwenyekiti wa mtaa.

Msigwa alisema hayo jana jioni Jumatano Juni 27,2019 katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la stendi kuu kata ya Miyomboni Kitanzini.

Alisema wananchi wa Iringa wanapaswa kuchagua mtu wanayemtaka na siyo kuruhusu kuchaguliwa na watu wachache.

Mchungaji Msigwa alisema katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia mtu wanayemtaka katika mitaa yao na kuwataka kuchagua wawakilishi wa Chadema na kuwagaragaza wa CCM.

“Tumejipanga vizuri Chadema katika uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo nawaomba mnapokwenda kuchagua chagueni wawakilishi wa Chadema katika mitaa yote ili tuwaonyeshe CCM kuwa bado Chadema iko imara,” alisema Mchungaji Msigwa

Mchungaji Msigwa aliwaeleza wananchi kuwa waliahidiwa laptop, maisha mazuri kwa wanyonge na  CCM lakini wametapeliwa kwani hazijatekelezwa.

Pia Soma

Kwa upande wake, Diwani wa Mivinjeni, Frank Nyalusi alisema wananchi wana akili ya kujua kiongozi bora hivyo sio sahihi kumtisha mwananchi ili achague kiongozi fulani.

Nyalusi alisema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinataka kuwarudisha wananchi katika ukoloni ambapo walikuwa wanalazimishwa kuwa chini ya mtawala wa mkoloni.

“Nchi hii ni nchi ya mfumo wa vyama vingi katika mfumo wa vyama vingi kunakuwa na demokrasi ambapo unachagua kiongozi unayemtaka hivyo niwaombe wananchi ifikapo uchaguzi wa serikali za mitaa kuchagua kiongozi mnayemtaka na sio kushinikizwa na mtu,” alisema Nyalusi

Chanzo: mwananchi.co.tz