Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Msigwa: Nitamkumbuka Magufuli kwa Mambo Haya

Msigwa?fit=700%2C464&ssl=1 Mchungaji Msigwa: Nitamkumbuka Magufuli kwa Mambo Haya

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mchungaji Msigwa: Nitamkumbuka Magufuli kwa Mambo Haya March 26, 2021 by Global Publishers



Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema atamkumbuka Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli kwa mambo makubwa matatu.

Mchungaji Msigwa ambaye leo Ijumaa Machi 26, 2021 ameungana na mamia ya watu mjini Chato Mkoa wa Geita katika mazishi ya Magufuli ameyataja mambo hayo kuwa ni kurejesha nidhamu kazini, uwajibikaji na uthubutu.

“Mimi ni Mkristo katika kipindi hiki nitamkumbuka kwa mazuri biblia imerekodi watu maarufu kwa mazuri na mabaya katika kipindi hiki nitamkumbuka kwa mazuri hayo,” amesema Msigwa akibainisha kuwa ameshiriki msiba huo kama sehemu ya wanafamilia na sio chama.

Katika uwanja wa Magufuli inakofanyika ibada ya mazishi, viongozi na wananchi wanaendelea kuwasili akiwemo katibu mkuu kiongozi Balozi Bashiru Ally, mawaziri, wabunge na viongozi wa CCM.

Chanzo: globalpublishers.co.tz