Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Kituni kukaimu nafasi ya Katibu Chadema Wilaya ya Serengeti

Wed, 18 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara. Siku chache baada ya Katibu wa Chadema Wilaya ya Serengeti Mkoa Mara Julius Anthony kujiuzulu kutokana na tuhuma za kuhujumu chama, nafasi yake imezibwa na mchungaji Zakaria Kituni.

Katibu wa chama Mkoa wa Mara Chacha Heche amesema baraza la chama mkoa limemteua mchungaji  Kituni kukaimu nafasi hiyo wakati uchunguzi ukiendelea dhidi ya aliyekuwa katibu wa chama wilaya.

"Katika kikao kilichoketi Julai 17,2018 wilayani Serengeti tulikubaliana kuweka kaimu ili shughuli ziweze kusonga ,wakati huo tunaendelea kuchunguza tuhuma zinazomkabili ikithibitika tutachukua hatua zaidi,” amesema Heche.

Kwa upande wake mchungaji Kituni amesema kazi yake ya kwanza ni kuleta umoja ndani ya chama ili kufikia malengo kusudiwa ya Chadema.

Akizungumza na mwananchi digital katibu aliyejiuzulu Anthony amesema  anabaki kuwa mwanachama wa kawaida, lakini wakiona hafai atakubaliana na uamzi huo .

Baadhi ya tuhuma zinazomkabili  ni kusababisha mgombea wa chama hicho Kata ya Ikoma kushindwa kurejesha fomu ya uteuzi kwa kumjazia fomu vibaya.

Chanzo: mwananchi.co.tz