Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezo wa kuhama hama vyama, CHADEMA wapata pigo lingine

1149 15241748 1325595460846006 8218755187414391136 N TZW

Fri, 5 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mchezo unaoendelea wa viongozi wa vyama vya kisiasa nchini Tanzania wa kuhama hama vyama bado umepamba moto kwani ikiwa zimepita siku mbili tu tangu Madiwani wawili wa Chadema huko Mkoani Iringa kutangaza kukihama chama hicho leo tena Januari 5, 2015 Diwani mwingine wa Chadema amehamia CCM.

Zakayo Chacha

Diwani huyo sio mwingine ni Diwani wa Kata ya Turwa, wilayani Tarime, Zakayo Chacha ametangaza kujiuzulu na kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM .

Soma na hii-‘Huwezi kumsifia Rais ukiwa nje ya chama chake’ – Madiwani waliohama CHADEMA kwenda CCM

Akieleza sababu za kuhamia CCM amesema kuwa ni kuvutiwa na kasi ya utendaji wa Rais Magufuli hivyo ameona hana budi kujiunga CCM ili aungane naye katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

Chanzo: bongo5.com