Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchakato wa uchaguzi Jimbo la Kwandika waanza

Kuraaa.png Mchakato wa Uchaguzi Jimbo la Kwandika waanza

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Jimbo la Ushetu, Emmanuel Mbamange leo ametangaza uchukuaji wa fomu za kugombea jimbo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na aliyekuwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Elias Kwandikwa.

Fomu hizo zimeanza kutolewa leo tarehe Agosti 30,2021 na kikomo chake kitakuwa Septemba Mosi saa 10:00 jioni na siku inayofuata itakuwa siku ya kupiga kura za maoni za kumtafuta mgombea.

Ikumbukwe kuwa Kwandika alifariki mapema mwezi Agosti katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live