Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchakato mpya kura ya maoni CCM huu hapa

Video Archive
Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Makamu mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula amesema mchakato wa kura ya maoni wa chama hicho tawala nchini Tanzania kwa ajili ya kusaka wagombea wa ubunge na udiwani utakuwa tofauti na miaka iliyopita.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Februari 8, 2020 katika kongamano la miaka 43 ya kuzaliwa kwa CCM lililofanyika mkoani Dodoma.

Amesema utaratibu utakaotumika mwaka 2020 itakuwa ni kuwachuja wagombea kabla ya kuingia kwenye mchakato wa kura za maoni.

Mangula amesema utaratibu wa kuwa na utitiri wa wagombea na kuwaruhusu waende kwenye maeneo ya wapiga kura, ulikuwa ni mwanya wa watu kutumia rushwa kusaka madaraka.

Amesema watakaokuwa vimbelembele ndio watakuwa wa kwanza kuwekwa kando.

Bila kueleza mfumo utakaotumika amesema hawawezi kupeleka watu wote katika uchaguzi, “na hilo lilichangia chama chetu kuingiza viongozi wala rushwa na wasiofaa.”

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz