Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge wa zamani CUF ajiuzulu, ahamia CCM

11815 MBUNGE+PIC TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pangani.Mbunge wa zamani wa viti maalumu mkoa wa Tanga (CUF),Amina  Mwidau ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kutangaza nia yake ya kujiunga na  CCM.

Kwa mujibu wa taarifa aliyosambaza kwenye vyombo vya habarin leo Julai 19, Mwidau ameeleza sababu ya kuhama CUF akidai anajipanga kivingine katika safari ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Amesema amechukua uamuzi huo ikiwa ni miaka miwili na nusu ya kutafakari mwenendo wa kisiasa ndani ya CUF vyama vingine vya upinzania pamoja na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano na hivyo ameamua kujivua.

“Nimeridhika sasa ni wakati muafaka wa kujipanga kivingine katika safari ya kushiriki kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi wote,”alisema Mwidau.

Mwidau aliyekuwa mbunge kuanzia wa viti maalum 2010 hadi 2015 pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) amesema ameamua kujiunga na CCM kwa sababu  bado anayo ndoto ya kuendelea kushirikiana na wananchi wote katika kuleta ustawi na maendeleo na hayupo tayari kuishia njiani.

Akizungumza jana, katibu wa CCM, Mkoa wa Tanga, Allan Kingazi amesema kuwa mapokezi ya Mwidau yatafanyika Jumamosi katika uwanja wa Makorora Katim.

 “Tutampokea kesho jumamosi Makorora jijini Tanga tumefurahi kwa sababu Mwidau ana nguvu hasa kwenye siasa za Wilaya ya Pangani.”alisema Kingazi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz