Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge wa Ngorongoro kujisalimisha leo

Iondoopic Mbunge wa Ngorongoro kujisalimisha leo

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda wowote kuanzia sasa Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel ole Shangai atajisalimisha kwenye Kituo cha Polisi jijini Arusha baada ya msako wa siku kadhaa.

Habari zinasema kuwa kwa siku kadhaa Polisi wamekuwa wakimtafuta Shangai ikiwemo kumpelekea wito huku pia wakidaiwa kufika nyumbani kwake.

Hata hivyo, Shangai amesema kuwa leo Jumatatu atafika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Arusha kukutana na Mkuu wa Upepelezi.

Hatua hiyo ya kujisalimisha kwake imetokana na kile kinachodaiwa kuwa mbunge huyo anatuhumiwa kuhusika na tukio la kushambuliwa waandishi wa habari lililotokea Agosti 15, 2023.

Waandishi hao walishambuliwa na wananchi kwenye mkutano uliofanyika eneo la Enduleni wilayani Ngorongoro.

"Nipo njiani na nakuja Arusha kuonana na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi mkoa Arusha (RCO) ili nifahamu sababu za kutafutwa hadi nyumbani kwa wazazi wangu tena usiku," amesema Shangai.

Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Justine Masejo hakupatikana kuzungumzia sakata hilo la Shangai ikielezwa kuwa yupo kwenye msafara wa Rais Samia Suluhu Hassan anayeshiriki maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live