Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge wa Kibiti ajenga hospitali, shule za CCM

IMG 5359 001 768x513 Mbunge wa Kibiti ajenga hospitali, shule za CCM

Mon, 27 Jun 2022 Chanzo: BBC

Mbunge wa Jimbo la Kibiti mkoani Pwani Twaha Mpembenwe baada ya kufanya ukarabati na kujenga majengo mapya kwenye hospitali, shule na ofisi za CCM jimboni humo juzi Jumamosi viongozi na wanachama wa CCM jimboni humo wamepokea vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa jengo la ofisi za wilaya hiyo.

Miongoni mwa vifaa hivyo ni gypsum board na vinginevyo kwa ajili ya kumalizia ofisi hiyo kutoka kwa wadau wa maendeleo jimboni humo Chama cha Ushirika mkoa wa Pwani (CORECU) katika kuunga mkono juhudi za Mbunge Mpembenwe ambaye sasa ameamua kuzivalia njuga ofisi za CCM jimboni na kutaka ziwe za kisasa.

Pamoja na CORECU naye mfanyabiashara wa Cosmas Sisa anayefanyia shughuli zake eneo Kibiti barabara ya Kilwa amechangia vifaa kadhaa vya ujenzi katika kumuunga mkono juhudi za Mbunge Mpembenwe.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kibiti, Muhidini Zakaria amesema;

”Leo tumekusanyika hapa kwa ajili ya kupokea vifaa vya ujenzi ikiwemo gypsum board na vinginevyo kwa ajili yakumalizia ofisi ya CCM wilaya ya Kibiti.

Muhidini amesema kuwa hizo zote ni jitihada za Mbunge wa Kibiti, Mh. Twaha Mpembenwe ambaye sasa ameamua kuwekeza nguvu kwa chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya matawi kata na wilaya.

“Alianzia kuunga mkono kwenye ngazi ya kata wilaya ambapo kata ya Mlanzi, Mtawanya, Mjawa na kwingineko ametoa mifuko mingi ya saruji na mabati ili zijengwe ofisi za chama kwa ajili ya maendeleo ya chama.

“Mbunge Mpembenwe amekuja na vipaumbele vya kutaka kulifanyia ukarabati jengo la CCM Wilaya ya Kibiti kwa kuweka bati mpya tiles, madirisha ya vioo fisherboard na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.

“Lengo la Mh Mpembenwe ni kutaka kuhakikisha hadi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM ngazi ya Wilaya mwezi September 21 tuwe tumemaliza jengo letu la CCM Wilaya ambalo tutalitumia kwa ajili ya vikao vya chama na miradi mbalimbali ya Chama.

Katika kumalizia jengo hilo, Mh Mpembenwe ametoa mifuko 600 ya saruji ambayo itasaidia kufyatua matofali 15,000 yatakyotumika kujenga ukumbi na uzio kwenye jengo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Pwani CORECU Mussa Mng’eresa amesema ofisi yake imeamua kutoa msaada huo wa gypsum ikiwa ni jitihada zao za kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa ilani ya CCM na Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Mh Twaha Mpembenwe.

Chanzo: BBC