Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge wa CCM aanza kuelimisha Corona

99166 CCM+PIC Mbunge wa CCM aanza kuelimisha Corona

Tue, 17 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Viti Maalumu, Mariamu Ditopile Mzuzuri(CCM) ameanzisha safari ya uelimishaji wa kujikinga na maambukizi ya ugonjwa unaotokana na virusi vya Corona (COVID-19). Mariam ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini waliofanya ziara jana katika Soko la Madini la Kimataifa Jijini Dar es Salaam ameonekana leo akiwa amevaa maski iliyoziba maeneo ya pua na mdomo kwa lego la kuelimisha watanzania kwa vitendo. Ziara hiyo chini ya Mwenyekiti wake Dastan Kitandula iliwakutanisha pamoja maofisa wa soko hilo la madini, Tume ya Madini Tanzania(TMC) pamoja na wafanyabishara wa madini kujadili, mafanikio na changamoto zinazowakabili kibiashara. Amesema alianza leo kuvaa na ataendelea kuivaa maski hiyo hadi pale serikali itakapotoa taarifa za hali ya salama. “Lengo ni kutahadharisha watanzania kuhusu virusi vya corona, kama tunavyosalimiana na miguu, kujisafisha mikono mara kwa mara basi kuvaa maski kwa sasa ni moja ya njia za kuchukua tahadhali hiyo,”amesema Mariam leo Machi 15, 2020 jijini Dar es Salaam. “Kwa sasa kila mtanzania anatakiwa kuzingatia taarifa zote za kujikinga, kwamba kinga ni nzuri kuliko tiba, unaweza kuvaa maski na shughuli zako nyingine zikaendelea,”

Chanzo: mwananchi.co.tz