Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge mwingine wa upinzani ajiunga CCM leo

11666 Pic+kuchauka TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Liwale kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Zuberi Kuchauka leo Jumatatu Agosti 13, 2018 ametangaza kujiunga na CCM.

Ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini hapa, akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Dk Bashiru Ally.

Kuchauka amesema moja ya sababu iliyomuondoa CUF ni utendaji kazi wa Rais John Magufuli pamoja na mgogoro unaokitafuta CUF.

CUF imekumbwa na mgogoro tangu Profesa Ibrahim Lipumba kurejea katika uongozi mwaka 2016, ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipojiuzulu uenyekiti wa chama hicho.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz