Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge awakalia kooni waliotafuna fedha za mikopo

Mwaifunga Pic Mbunge awakalia kooni waliotafuna fedha za mikopo

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Mwaifunga amewakalia kooni watu waliokula fedha za asilimia 10 zinazotolewa na halmashauri nchini kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu akiwataka wazirejeshe.

Mwaifunga ameyasema hayo Jumatatu Aprili 17, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2023/2024.

Amesema si kweli fedha hizo zimepotea kwasababu kuna maeneo wayokwenda wakakuta kikundi cha familia kikiwa na baba, mama na watoto wa baba mkubwa.

Amesema kikundi hicho kilipewa Sh30 milioni lakini walivyowahoji wanafanya biashara gani hakuna aliyeweza kusema ni biashara gani wanayofanya.

Amesema hata walipomhoji ofisa maendeleo ya jamii kuwa wakati alipokwenda kukagua hakulioa hilo, hakuweza kujibu.

“Tunataka fedha zirudi, wapelekwe wataalamu wa fedha kabla ya kutoa fedha kwenye vikundi. Maofisa maendeleo hawana utaalam ndio maana wameshindwa kwashauri wananchi wetu,”amesema.

Amesema maofisa wa fedha wataweza kuwashauri wananchi ni biashara gani wanaweza kufanya ili waweze kurudisha marejesho ya fedha hizo.

“Baadhi ya maofisa maendeleo wanachukua fedha hizi kwa kisingizio wanakwenda kuwapa vikundi, ndo maana tunasema fedha hizi lazima zirudi,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live