Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge atishia kuondoka na Siwa ya Bunge kisa Anwani za makazi

Makazi Anuani Mbunge atishia kuondoka na Siwa ya Bunge kisa Anwani za makazi

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Mbinga vijijini (CCM), Benaya Kapinga ametishia kuondoka na Siwa ya Bunge endapo fedha za barabara zilizochukuliwa jimboni kwake kwa ajili ya mchakato wa anuani za makazi hazitarejeshwa.

Ameyasema hayo bungeni alipokuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema barabara hizo zinahudumia wananchi wa kata nne ambao kwa sasa wanalazimika kwenda umbali wa kilometa 30 kufuata huduma ya hospitali, na kuhoji kwanini katika Wilaya ya Mbinga kumefanyika utaratibu huo.

“Hivi kati ya barabara na mabao kipi ni muhimu zaidi? Hivi ni nani anaweza kuvumilia kukosa kibao na kukosa kupita njia nzuri kwenda hospitali? Barabara hizi zina mashimo, mawe haipitiki sasa hivi wananchi wanalazimika kwenda Mbinga kilometa zaidi ya 30 wakati hapo ni kilometa 10 tu,” amesema.

Ameongeza “Pamoja na uzuri wa mradi huu pamoja ninaheshimiana na Mheshimiwa Nap,e ninataka kwenye majumuisho aeleze fedha hizi zitarejeshwaje na miradi hii itatekelezwaje. Bila hivyo nitaondoka na Siwa hii, haiwezekani, hili Siwa nitatoka nalo, lazima aniambie Mheshimiwa Nape.”

Kufuatia kauli hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, uratibu na Bunge), George Simbachawene amesema Siwa ndiyo Bunge lenyewe kwa mujibu wa utaratibu wa mabunge ya Jumuiya ya Madola na heshima ya bunge pia, hivyo atakuwa mbunge wa kwanza kufanya hivyo kwa kuwa hakuna aliyewahi kuondoka na Siwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live