Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka wagogo wafundishwe matumizi ya zebra

15647 Pic+wagogo TanzaniaWeb

Wed, 5 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Mtwara Mjini (CUF) Maftaha Nachuma ameitaka Serikali kuwapa elimu wagogo juu ya matumizi ya zebra wakati wanapovuka barabara kwa sababu watu wamekuwa wakikatiza barabara kama wanaelekea ndani kwao.

Akichangia Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa mwaka 2018, leo Septemba 4 2018, Nachuma amesema katika zebra zilizopo jijini hapa wagogo wamekuwa wakivuka kama hawataki.

“Ukiwa unaendesha gari wagogo wanataka kukatiza katika zile zebra wanakatisha kama hawataki. Mheshimiwa Spika kuna hatari kubwa sana kwa kuwa tumehamishia makao makuu hapa, wagogo wapewe elimu,”amesema.

Amesema watu wanaovuka barabara jijini hapa wmekuwa wakikatisha kwenye vivuko kama wanaingia ndani (nyumbani kwao).

“Zebra siyo ina maana watu watembee kilojo lojo Mheshimiwa Spika. Itolewe elimu kuwa wakimbie wakati wanakatisha maeneo ya zebra. Kwa mujibu wa Sheria ya barabarani zebra mwisho ni saa 12 jioni wakivuka usiku wanatakiwa kukimbia kwa sababu ya kuepuka kugongwa,”amesema.

Aidha, Nachuma amesema waendesha baiskeli wa jijini hapa wamekuwa hawajali watembea kwa miguu wala magari na kuiomba wizara inayohusika kutoa elimu ili wagogo wasigongwe gongwe.

Pia ametaka kuboreshwa kwa maeneo ya Dodoma kwa kujenga miundombinu na kwamba kuna maeneo mengine mvua ikinyesha hayapitiki.

“Kuna maeneo mengine hapa karibu tu wakati wa mvua waheshimiwa wabunge walikuwa wakiacha magari yao kama mita 200 na kutembea kwa miguu kuelekea nyumbani,”amesema.

Pia ametaka kuongezwa kwa watumishi wa ardhi ili wanaoomba vibali vya ujenzi wasichukue muda mrefu.

Chanzo: mwananchi.co.tz