Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka makufuli ya TRA yatupwe

Mon, 17 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Makambako (CCM) Deo Sanga ametaka makufuli ambayo yalikuwa yakitumiwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kufunga biashara yatupwe.

Akichangia mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020,leo Jumatatu Juni 17 2019, Sanga amesema hilo litawapa matumaini wafanyabiashara nchini.

“Niipongeze Serikali kwa kupiga marufuku TRA kufungia biashara lakini niombe makufuli yaliyokuwa yakitumika kufunga biashara ahuko wilayani na mkoani yatupwe,”amesema.

Wakati huohuo, Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa ameitaka Serikali na mawaziri waliopewa dhamana waache siasa kwenye kilimo cha pamba.

Akichangia mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020, leo Jumatatu Juni 17 2019, Ndassa amewataka mawaziri hao ni wale waliopewa dhamana ya kusimamia Kilimo na yule wa Viwanda na Biashara.

“Kinachotokea sasa kuna mawakala wako kule ambao wanasema sisi tunazo pesa watanunua kwa Sh1,200 kila kilo ya pamba, lakini wanawapa watu wao wanaenda kununua kwa Sh 700,” amesema.

Pia Soma

Amesema kwa bahati nzuri Serikali inawafahamu na kwamba wamekuwa wakichezea wakulima na kuwanyanyasa wakulima wa zao hilo.

Amesema kama pamba itakaa katika maghala bila kununuliwa mwathirika wa kwanza atakuwa mkulima na halmashauri kwa kushindwa kupata kodi ushuru.

Chanzo: mwananchi.co.tz