Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataja sababu kujitoa kugombea na Lissu

89212 Mwakagenda+pic Mbunge ataja sababu kujitoa kugombea na Lissu

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Sophia Mwakagenda,  Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) ameeleza sababu za kujitoa kugombea umakamu mwenyekiti wa chama hicho (Bara) na kumuacha Tundu Lissu kuwa mgombea pekee.

Mbunge huyo alijitoa dakika za mwisho wakati akiomba kura za wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam kuanzia jana asubuhi  Desemba 18, 2019 na kuhitimishwa leo alfajiri Alhamisi Desemba 19, 2019.

Amesema alichukua uamuzi huo kwa kuwa yeye ni fundi wa kupiga chenga lakini Lissu ni mkali wa kufunga magoli.

Kutokana na kutojitoa mapema karatasi za uchaguzi zilikuwa zimeandaliwa na alipigiwa kura 11 huku Lissu akipata kura 930 sawa asilimia 98.8.

Akizungumza na Mwananchi leo Mwakagenda amesema, “ukiwa fundi na kamanda unayepanga jeshi lako ni lazima uhakikishe una safu iliyokamilika, ndio maana nikasema nimeshacheza mechi dakika 90 tunaingia kwenye matuta. Mimi ni fundi wa chenga,  Lissu  ni mtaalamu wa magoli nikaamua kumuachia.”

"Mheshimiwa mwenyekiti (Freeman Mbowe) nakupongeza  sana makamu mwenyekiti Zanzibar (Said Issa Mohammed) nakupongeza pamoja na Lissu. Nazipongeza safu za mabaraza yote nawaambia tunakwenda kupambana," amesema Mwakagenda.

Amesema atahakikisha anatoa ushirikiano na kuwaunga mkono viongozi wote waliochaguliwa, “watu 11 walionipigia kura ni tiketi kuwa kuna kitu mmekiona katika utendaji wangu. Nitahakikisha ninaitunza hii imani na kuiendeleza kwa kuchapa kazi kwenye ubunge wangu.”

Chanzo: mwananchi.co.tz