Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge apinga matokeo la saba

Tue, 18 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shirika la kupambana na uhalifu nchini Uingereza(NCA), limezionya shule binafsi na kutaka zitoe taarifa haraka polisi ikiwa wazazi watajaribu kulipa ada ya watoto wao kwa fedha tasilimu, ili kupambana na utakatishaji wa fedha.

Mkuu wa Shirika hilo Donald Toon alisema shule binafsi zinatakiwa kuwa na uangalifu kwa kuwa inawezekana mlipaji akawa kwenye orodha ya vitendo vya uhalifu. Alisemaa kuwa shule binafsi zina viashiria vya kiwango cha juu cha kutumiwa na wahalifu.

Aidha, alisema watunza fedha wanatakiwa kuwa waangalifu na kuwa hata shule za umma tayari zimechukua tahadhari kwa kukataa malipo ya aina hiyo ambayo yanaweza kuziingiza kwenye vitendo vya utakatishaji wa fedha.

Hata hivyo, alisema hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa kuna shule iliyopokea malipo yasiyofaa na kuwa hategemei kama shule zenyewe zitafanya uchunguzi wake binafsi ili kujua chanzo cha fedha zinazolipwa shuleni na wazazi.

Alisema hatua hiyo haina lengo la kuziumiza shule hizo na kuwa hawasemi kuwa waanze kuchunguza vyanzo vya mapato ya wazazi lakini kabla ya kupokea malipo yoyote ni muhimu kupitia historia ya mlipaji kama hana uhusiano wowote na mitandao ya kihalifu.

Kauli hiyo inafuatiwa na onyo lililotolewa na Waziri wa usalama mwezi mmoja ulipita kuwa shule binafsi, klabu za mpira, mawakala na wafanyabiashara wa magari ya anasa, ni maeneo yanayotakiwa kufuatiliwa kwa karibu baada ya kuhusishwa na vitendo vya utakatishaji wa fedha.

(The Telegraph, picha na BBC)



Chanzo: mwananchi.co.tz