Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge apinga Uhamiaji kuwa jeshi

WhatsApp Image 2021 09 08 At 4.50.43 AM.jpeg Mbunge apinga Uhamiaji kuwa jeshi

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

MBUNGE wa Viti Maalum, Agnesta Lambert, ameonesha mashaka yake kuhusu Muswada wa Sheria wa kuibadili Idara ya Uhamiaji kutambulika kuwa jeshi kwa kuwa inaharibu taswira ya nchi kidiplomasia.

Akichangia Leo kwenye Muswada wa Sheria ya Marekebisho namba tano wa mwaka 2021, Mbunge huyo amesema suala hilo halipo sawa na inahitaji idhini ya kutoka kwa Amri Jeshi Mkuu.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George  Simbachawene, amesema suala la Idara hiyo kuwa Jeshi kamili ni jambo la kawaida hata Mataifa makubwa ikiwemo Uingereza,  Marekani, India na Australia,  idara ya uhamiaji ni jeshi kamili.

Chanzo: ippmedia.com