Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge amshauri wenzake kuondoka na siwa

Siwa Pichnjnj Mbunge amshauri wenzake kuondoka na siwa

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Jacqueline Msongozi amewashauri wenzake waondoke na siwa hadi hapo Serikali itakapokwenda kulichukua Ruvuma na kujenga madarasa ya Shule ya Songambele wilayani Nyasa.

Mbunge huyo alitoa hoja hiyo jana Jumatatu Aprili 17, 2022 wakati akitoa taarifa kwa Mbunge wa Nyasa (CCM), Stella Manyanya aliyekuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2023/2024.

Awali Manyanya alisema kuwa kuna Shule ya Songambele ambayo aliitembelea na kukuta madarasa mawili yaliyokuwa pamoja yana nyufa na yana hali mbaya na watoto walikuwa wanaingia wanacheza.

“Nikataka madarasa hao yabomolewe kwa usalama wa watoto halafu tuendelee na ujenzi, hadi mpaka leo na nimeandika barua chungu mbovu (nyingi) kwenye wizara (Tamisemi), bila kusikilizwa, mlitaka nifanyeje? Angekufa kwanza mtu ndio niwaambie,”amesema.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akizitafuta fedha kwa gharama na kutaka fedha hizo zitendewe haki.

Baada ya kauli hiyo, alisimama Jacquline akimpa taarifa Manyanya ambapo amesema jambo hilo limekuwa likijirudia na amekuwa akiomba mara kwa mara bila kusikilizwa.

“Kwa sababu umekuwa ukiomba, husikilizwi unaonaje sisi kama wana-Ruvuma tuondoke na siwa hapa mpaka siwa hilo lije lifuatwe Ruvuma na darasa hilo liwe limeshajengwa,”amesema.

Akijibu taarifa hiyo, Manyanya alimshukuru na kumsihi mbunge huyo wasiondoke na siwa kwa sababu kwa kufanya hivyo maana yake Bunge litakuwa limesimama na watakuwa wamekosa kisheria.

Chanzo: mwanachidigital