Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge alia na ubakaji jimboni kwake

15485 Mbunge+pic TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Chwaka (CCM) Bhagwanji Maganlal amesema jimbo lake limekuwa likikabiliwa na tatizo la ubakaji na kuhoji ni lini Serikali itapeleka gari kwa ajili ya doria ya polisi ili kukabiliana na tatizo hilo.

“Je ni lini Serikali itapeleka gari ‘radio call’ pamoja na vitendea kazi vingine katika kituo cha Polisi cha Chwaka na Jozani?”amehoji mbunge huyo bungeni leo Septemba 4, 2018.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema mchakato wa ununuzi wa magari mapya ya polisi utakapokamilika watazingatia vigezo na iwapo watakidhi watapelekewa gari.

“Mchakato wa ununuzi wa magari utakapokamilika na kama itakidhi vigezo basi watapelekewa. Mheshimiwa mbunge avute subira hadi yatakapopatikana,”amesema.

Amesema mgao wa magari utazingatia kiwango cha uhalifu katika eneo husika, idadi ya watu na ukubwa wa eneo la doria.

“Kituo cha Polisi Chwaka kinatumia mawasiliano ya radio za mikononi. Aidha radio ya mezani kwa ajili ya kituo cha polisi Jozani imekwishapatikana na mafundi wa radio za polisi wanamalizia ufungaji wake kurejesha mawasiliano ya uhakika katika eneo hilo,”amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz