Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge akumbushia mpango wa Ukonga kuwa Wilaya

MBUNGE 222 Mbunge akumbushia mpango wa Ukonga kuwa Wilaya

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Mbunge wa viti maalum Mariam Kisangi, ameihoji serikali kuhusu mpango wa jimbo la Ukonga kuwa wilaya ili kuwasogezea huduma wananchi wa maeneo ya Msongola, Chanika na Zingiziwa kwani wanapata tabu kufuata huduma kwenye ofisi ya Manispaa ya Halmashauri ya wilaya ya Ilala zilizopo mjini.

Submitted by Agnes Kibona on Alhamisi , 24th Jun , 2021 Mbunge wa viti maalum Mariam Kisangi

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 24, 2021, Bungeni Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu, swali ambalo lilielekezwa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kujibiwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo David Silinde.

"Je serikali ina mpango gani wa kuanzisha wilaya mpya ya Ukonga katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, kwa kuwa mchakato wa kuanzisha wilaya ya Ukonga ulifanywa 2015 sambamba na uanzishwaji wa Wilaya ya Kigamboni na Ubungo ambazo wakati huo mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na Halmashauri tatu, na wilaya hizo zote zilifanya mchakato wa kuongeza Halmashauri," aliuliza mbunge huyo.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde alisema "Kama kuna nia ya kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Ukonga, anzeni upya mchakato mfuate taratibu zote za kisheria, mlete maombi na sisi tutayapeleka kwa Mhe.Rais na yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ya kuanzishwa wilaya mpya ama kusitisha kwa kadri atakavyoona inafaa".

Chanzo: eatv.tv