Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge aitaka Serikali ya Tanzania kupeleka bungeni taarifa za kutosha

64634 Salehe+pic

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Malindi (CUF) nchini Tanzania, Ally Salehe ameitaka Serikali ya Tanzania inapoleta hoja bungeni kuwa na taarifa za kutosha kwa sababu kizazi cha sasa kinaweza kutafuta taarifa kupitia mitandao.

Salehe ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Juni 27, 2009 wakati wakichangia Muswada wa Marekebisho wa Sheria mbalimbali namba 3 kwa mwaka 2019.

Mbunge huyo amesema kumekuwa na maboresho katika kifungu hicho na anadhani wamewasikiliza Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia (WB).

Amesema mabadiliko ya sheria hiyo yanatenganisha takwimu za utafiti na tathimini eneo ambalo lilikuwa na utata katika sheria ya takwimu.

Salehe amesema wamejaribu kutenganisha viwango vya kimataifa na nchini na kusiwe na tofauti kubwa sana kati ya kimataifa na kitaifa.

“Kwa sababu takwimu kama sayansi ina vigezo vilevile, unaweza kuvitumia lakini kingine ni namna ya mtu yoyote anaweza kutoa takwimu na (Ofisi ya Taifa ya Takwimu) NBS watakuwa na haki ya kujibu takwimu hizo,” amesema.

Pia Soma

Amesema pia Serikali ya Tanzania imefanya jambo jingine zuri la kuunda kamati ya ufundi ambayo itakuwa na jukumu la kutazama kama takwimu zinaenda sawa ama la kwa maana kama zimetimiza masharti ya kisayansi.

Salehe amesema anakubaliana na kuletwa kwa hati ya dharura lakini wamewabana sana kwa kuweka siku chache za kamati kujadili marekebisho hayo ya sheria nane.

Amesema hakuona sababu kubwa ya kufanya dharura hiyo kwa sababu wangeweza kuzileta wakati ujao.

Amesema wapinzani hawapigi ila wanashauri namna ya kutengeneza sheria ambazo zitakuwa bora na rafiki kwa wawekezaji wanaokuja nchini.

“Unakuwa na kizazi kipya cha wabunge, wabunge ambao wanaweza kugeogle, wanaweza kufanya utafiti… ije na taarifa za kutosha ili ziweze kutusaidia,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz