Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge aitaka Serikali kukamilisha miradi ya maji Ushapu

Lucy Mayenga Mbunge aitaka Serikali kukamilisha miradi ya maji Ushapu

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti maalum CCM mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga ameitaka Serikali chini ya Wizara ya Maji kukamilisha miradi inayosuasua katika eneo la Ushapu ambapo ujenzi wake umekwama kuendelea kutokana na tatizo la fedha.

Mhe Lucy Mayenga ameyasema hayo hii leo wakati akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya maji Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa "Mheshimiwa Mwenyekiti nasema hivyo kwani kwangu kule kuna miradi ambayo imekwama kutokana na changamoto kubwa ya fedha hivyo kutokana na uwepo wa fedha hizi utasaidia kukamilika kwa miradi hiyo"

"Mheshimiwa Waziri sitokuelewa kama miradi ya Igaga, Lagana na miradi ya visima virefu itaendelea kukwama maana pesa mtakuwa tayari mnazo" amesema Lucy Mayenga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live