Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ahoji ziko wapi Noah za Watanzania

60015 Pic+heche

Tue, 28 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amehoji Noah zilizotajwa wakati wa serikali ilipodai fedha zilizokuwa zitolewe na kampuni ya migodi ya madini.

Akichangia mjadala katika hotuba ya Wizara ya Madini bungeni leo Jumatatu Mei 27, 2019, Heche amesema bado wananchi wanasubiri Noah ili Watanzania wazipande.

Siku za hivi  karibuni, Serikali ilipitia baadhi ya mikataba ya madini na kubaini kulikuwa na mapunjo ya malipo ya mirabaha na tozo mbalimbali ambazo baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa fedha zake zingeweza kununua Noah moja kwa kila Mtanzania. Amesema Watanzania wana macho, wana masikio na wanaweza kupambanua mambo hivyo, wanataka kujua Noah zao ziko wapi. Amezungumzia suala la malipo ya faini kwa kampuni za migodi kuwa ulipaswa kuelekezwa kwa wananchi kwa kuwa ndiyo waathirika.

Heche amesema tangu mwaka 2007 kumekuwa na kelele nyingi kuhusu utiririshaji wa maji katika migodi mingi ikiwemo Mara, lakini hakuna mtu anayejali.

Chanzo: mwananchi.co.tz