Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ahoji mkandarasi kuondoa vifaa

50628 Pic+mkandarasi

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga amesema mkandarasi anayejenga barabara ya Kidatu hadi Ifakara ameondoa vifaa baada ya Rais John Magufuli kuzindua ujenzi wa barabara hiyo mwaka jana.

Akiuliza swali la nyongeza Mlinga amesema mkandarasi huyo alileta vifaa vingi na Rais alipoondoka wakaondoa vifaa vyote.

“Ni lini wataanza ujenzi ama ni changa la macho kwetu sisi na mheshimiwa Rais,” amehoji.

Akijibu Naibu Waziri wa Ujenzi, Atashasta Nditiye amesema ni kweli kulikuwa na changamoto vifaa na material kwenye ujenzi.

Hata hivyo, amesema changamoto hiyo imekwisha na ujenzi wa barabara hiyo sasa utakwenda kwa kasi na wananchi wategemee kupata huduma bora.



Chanzo: mwananchi.co.tz