Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge adai Rais Mstaafu Zanzibar anaishi kwenye hali ngumu

Mbunge Adai Rais Mstaafu Zanzibar Anaishi Kwenye Hali Ngumu Mbunge adai Rais Mstaafu Zanzibar anaishi kwenye hali ngumu

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Suleiman Haroub Suleiman amesema Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma anaishi katika hali ngumu baada ya nyumba yake kukabiliwa na mmomonyoko wa udongo.

Dk Salmin aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar katika kipindi cha kuanzia Oktoba 25 mwaka 1990 hadi Novemba 8, mwaka 2000.

Akiuliza swali bungeni leo Ijumaa Aprili 19, 2024, Suleiman amesema kuna baadhi ya viongozi ambao waliitumikia Serikali ya Tanzania akiwamo Dk Salmin ambaye anaishi katika hali ngumu.

Amesema ugumu huo unatokana na nyumba yake kukabiliwa na mmomonyoko wa udogo kwa sababu ipo karibu na bahari.

“Je, Serikali iko tayari kushirikiana na viongozi wa kamati ya baraza kuu la wawakilishi Zanzibar ili kutatua changamoto hiyo,” amehoji Suleiman.

Pia amesema kuna baadhi ya maeneo yanahitaji kutunzwa lakini hadi sasa yako katika hali hatarishi, ikiwemo shule aliyosoma Karume pasipo kueleza anamzungumzia Karume yupi.

Ofisi yake inashirikiana vizuri na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar wanalichukua na kujadiliana kuona wanafanyaje kuboresha maeneo hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live