Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge aangua kilio "watu sita wameuawa Jimboni akiwemo ndugu yangu"

WhatsApp Image 2021 11 12 At 16.jpeg Mbunge aangua kilio

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amemeomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kukutana na Mbunge wa Mbogwe Nicodemas Maganga (CCM) ilikutafuta suluhu ya mgogoro kati ya serikali na wananchi ambao sasa umesababisha vifo vya watu sita.

Mbunge wa Mbogwe, aliomba muongozo wa Spika akidai kuwa kumekuwa na mgogoro katika jimbo lake kuhusu sehemu ya uchimbaji madini na kwamba kesi iliyofunguliwa katika mahakama kutatua mgogoro huo imekuwa ikipigwa karenda.

“Kwanini wananchi wangu wamekufa mpaka sasa hivi sita amabao walikuwa wanadai haki zao,” amesema Maganga. “Kupitia mahakama ya Shinyanga imekuwa ikitoa hukumu kinyume cha sheria ...kuna hukumu karibia tatu ambazo zimesababisha wananchi wangu wafe.”

Maganga amedai kuwa alipata ushawishi kutoka kwa watu wa madini waliojitambulisha kuwa wao ni mafisa usalama wako kwenye system, hata hivyo alikataa kwa rushwa kukuwa mmoja kati ya walifariki ni Binamu yake.

Hata hivyo Kabla ya Ndugai kutoa muongozo, Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde (CCM) alishauri Bunge kuunda kamati maalum kuchunguza mgogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama aliomba Waziri wa Madini Dotto Biteko kupewa nafasi ya kueleza kuhusu mgogoro huo lakini spika alisema ni busara Waziri Mkuu kuangalia namana anavyoweza kutana na Waziri wa Madini pamoja na Mbunge ambao wote ni wanatoka mkoa wa Geita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live