Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Zungu adai Supermarket zinauza sabuni feki

ZUNGU WEB Mbunge Zungu adai Supermarket zinauza sabuni feki

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu, ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara, kuhakikisha inafanya uchunguzi na ukaguzi kwenye Supermarket zote kubwa nchini kwa kile alichodai kuwa nyingi zimekuwa zikiuza sabuni feki za kuogea.

Submitted by Agnes Kibona on Jumatano , 16th Jun , 2021 Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu

Zungu ametoa kauli hiyo leo Juni 16, 2021, Bungeni Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Viwanda na Biashara.

"Wizara ya Viwanda na Biashara hebu tumeni watu wenu kwenye Supermarket kubwa, Dettol na sabuni za kuogea zote ni 'fake' watu wanalipa pesa nyingi wanatumia vitu siyo halali na pesa wanazolipa, chunguzeni Supermarket zote, kama Dettol ukiitia maji inakuwa nyeupe lakini leo ukiitia maji inakuwa nyeusi pamoja na sabuni ambazo zimeandikwa majina makubwa pia ni feki," amesema Mh. Zungu.

Chanzo: eatv.tv