Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge: Zanzibar haikushirikishwa Dodoma kuwa jiji

15509 Dodoma+pic TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Malindi (CUF) Ally Saleh amesema Zanzibar haikushirikishwa katika uandaaji wa Muswada wa Sheria ya Kutangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018.

Akizungumza katika mjadala wa muswada huo bungeni leo Jumanne Septemba 4, 2018, Saleh amesema kumekuwa na utaratibu wa kutowashirikisha Zanzibar katika sheria zinazohusu Muungano na ndio maana zimekuwa zikikataliwa na Baraza la Wawakilishi. 

"Mfano  Sheria ya deep sea ( bahari kuu) ilipitishwa kimabavu hapa ikaenda kule Baraza la Wawakilishi ikakataliwa," amesema.

Hata hivyo, Spika wa Bunge Job Ndugai mara baada ya mbunge huyo kumaliza kuzungumza, alimjibu kuwa waliopo bungeni ni  wawakilishi wa wananchi wa pande zote mbili za Muungano.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz