Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Peneza aomba Rais Magufuli akubali maridhiano

94492 Pic+peneza Mbunge Peneza aomba Rais Magufuli akubali maridhiano

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema),  Upendo Peneza amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kukubali kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani kujadiliana kuhusu maridhiano kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020.

Ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Januari 5, 2020 katika mjadala wa taarifa za kamati za Bunge za  Utawala na Serikali za mtaa, Katiba na Sheria pamoja na Sheria ndogo.

“Nichukue nafasi hii kutoa shukrani zangu za pekee kwa Rais wa Tanzania kwa kauli kuwa uchaguzi mwaka 2020 utakuwa wa uhuru na haki,” amesema Upendo.

Upendo ameomba Serikali kufanya mabadiliko katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kwa kuwaondoa wakurugenzi waliopo ili kuwe na uchaguzi wa haki na uhuru.

Upendo amesema aliunga mkono kauli ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuhusu ombi lake la kutaka yawepo maridhiano ya kitaifa ili kuondoa changamoto zilizopo.

Amesema mwenyekiti huyo juzi ameonyesha nia ya kufikia maridhiano kwa kuandika barua kwa Rais Magufuli kuomba kukutana ili kuzungumza mambo mbalimbali.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

 “Lakini yeye (Mbowe) ametumia busara kuwa sasa wazungumze kabla ya maafa hayajatokea. Kwa busara hiyo namuomba mheshimiwa Rais atumie busara hiyo tukae chini tuzungumze twende mbele tufanye uchaguzi wa haki ili Amani tunayohitaji iweze kudumu ,”amesema.

Amesema hakuna kitendo cha uzalendo zaidi ya kuitakia nchi Amani na kwamba maridhiano ni kitendo cha uzalendo mkubwa sana.

Chanzo: mwananchi.co.tz