Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Nkamia adai jimboni kwake kuna njaa

77962 Nkamia+pic

Tue, 1 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Chemba (CCM) nchini Tanzania, Juma Nkamia amedai wananchi wa jimbo hilo wamebaki na njaa baada ya kutakiwa kumwaga vyakula kutokana na madai ya kuwa na sumu kuvu.

Nkamia aliyewahi kuwa naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 katika uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa kilimo cha matunda na mbogamboga.

Hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kkuibua madai hayo dhidi ya Serikali, amekuwa akieleza kuhusu wananchi wake kukabiliwa na njaa baada ya kutakiwa kumwaga vyakula vyao vinavyodaiwa kuwa na sumu kuvu.

Ugonjwa wa sumukuvu umekuwa ukijirudia katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma kusababisha vifo vya watu katika maeneo hayo.

"Serikali ilikuja kuwalazimisha wananchi kumwaga chakula, watu walimwaga mahindi magunia mengi lakini leo wanalia njaa,  Serikali haina mpango nao na kutuachia mimi na mbunge mwenzangu wa Kondoa (Dk Ashatu Kijaji- ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango), siyo jambo jema," amesema Nkamia.

Nkamia amesema gharama za mahindi zimefikia hadi Sh70,000 kwa gunia hivyo wananchi wengi hawawezi kuzimudu.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz