Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Mwakajoka, wanachama Chadema wakamatwa na polisi

11426 Mbunge+pic TanzaniaWeb

Sun, 15 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya.  Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka amekamatwa na Polisi akiwa kwenye kituo kikuu cha polisi Tunduma alikokwenda kuomba ulinzi.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumamosi Julai 14, 2018 mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga amesema mbali na Mwakajoka, pia Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo naye amaekamatwa.

“Pia wapo baadhi ya madiwani, wanachama wa Chadema na walinzi wa chama nao wamekamatwa,” amesema.

Amesema Mwakajoka na Sikagonamo leo asubuhi  walipanga kwenda ofisi za Halmashauri ya Tunduma kwa ajili ya kuchukua fomu za wagombea wa udiwani katika kata tano, lakini ofisi hizo zilikuwa zimezingilwa na polisi.

“Kutokana na hali hiyo Mwakajoka akiwa na Sikagonamo waliona kuliko kwenda eneo hilo na kuonekana wanakwenda kufanya vurugu, waliamua kwenda kuonana na mkuu wa kituo ili awape ulinzi wa askari,” amesema Hainga.

“Ila walipofika (Mwakojoka) alielezwa kuwa jana usiku alifanya kikao na wenzake kwa lengo la kufanya maandamano hivyo anawekwa chini ya ulinzi, basi wakawekwa ndani hadi muda huu.”

Amesema hatua waliyoichukua ni kuwasiliana na uongozi wa juu wa chama hicho sambamba na kufanya taratibu za dhamana.

Haonga amesema hadi leo saa 7 mchana hakukuwa na mgombea udiwani wa Chadema aliyechukua fomu  ya kugombea kwa kile alichokiita mizengwe inayofanyika, ikiwa ni pamoja na kukamatwa lwa wagombea walioteuliwa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

MCL Digital ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange kuzungumzia suala hilo amesema atalitolea ufafanuzi baada ya kupata taarifa kamili kwa kwa yupo nje ya ofisi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz