Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Jimbo la Konde Ajiuzulu

Screenshot 2021 08 02 At 13.png MBUNGE mteule wa jimbo la Konde, Sheha Mpemba Faki

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa masikitiko barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpeka Faki leo August 02, 2021

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 2 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, Faki ameandika barua ya kujiuzulu ambapo ameeleza kufikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia.

Shaka amesema chama hakina uwezo wa kumzuia katika uamuzi wake huo hasa ikizingatiwa ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM na kuwaomba wanachama wote kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati wakisubiri taratibu nyingine.

Amejiuzulu kabla hajaapishwa na Spika wa Bunge zikiwa zimepita siku 14 tu tangu alipochaguliwa katika uchaguzi uliohusisha pia chama cha ACT-Wazalendo ambacho kilipoteza jimbo hilo.

Faki alichaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 18 ambapo CCM ilishinda katika jimbo hilo pamoja na kata sita zilizoshiriki uchaguzi huo ambapo ilishinda bila kupingwa katika kata nne miongoni mwa hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live